Thursday, July 5, 2012

Kocha Thom Sainfiet (kushoto) na mmoja wa wagombea nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Peter Haule, wakifuatilia mazoezi ya timu hiyo. Beki wa Kijitonyama Stars, akipiga mweleka baada ya kupigwa chenga na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, kwenye mazoezi hayo. Mwanachana wa Yanga, Abdalah Bin Kleb (kulia) akimueleza jambo kocha.
 Peter Haule akimpeleka kocha kwenye gari aliloandaliwa kuondoka nalo baada ya mazoezi. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Magari (kushoto) akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Hamis Kiiza na Kipa Yaw Berko (kulia). Kocha akijiandaa kuingia kwenye gari aliloandaliwa.
WACHEZAJI wa  kikosi cha Yanga leo walifanya mazoezi ya kujituma kwa hali na mali katika Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ili kuonyesha uwezo wao kwa kocha mpya wa timu hiyo, Thom Sainfiet,  aliyefika uwanjani hapo kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo kwa mara yake ya kwanza.

No comments:

Post a Comment