Sunday, July 8, 2012

BIFU KATI YA IRENE UWOYA NA FLORA MVUNGI LA PAMBA MOTO





Irene Uwoya.

Flora Mvungi.

WASANII wa filamu ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa katika vita ya kurushiana maneno makali, Irene Uwoya na Flora Mvungi wamepondwa na wadau kuwa wanachokifanya kinawashushia heshima mbele ya jamii.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyati tofauti, wadau hao wamesema wameshangazwa na hatua ya wasanii hao ‘kuchambana’ kisa kikiwa ni penzi la mwanamuziki, Hamis Baba ‘H-Baba’.
Walisema kitendo cha kufikia kutukanana matusi ya nguoni kinaashiria wote hawana busara na kama wanatafuta umaarufu, wamepotea njia.
“Eti wanafikia hatua ya kuanikana mambo ya chumbani na kutukanana halafu wanajiita kioo cha jamii, huu ni ulimbukeni uliopitiliza,” alisema Mariam wa Kinondoni jijini Dar.
Naye Rashid Magole wa Mbezi alisema, ni vyema kama wawili hao wana tofauti wakakaa na kuzimaliza kuliko kuanza kuchanana kwani kuendelea kufanya hivyo kutawafanya wakose mashabiki.

No comments:

Post a Comment