HABARI za chini kwa chini zinadai kuwa, staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson (pichani) amefunga ndoa huko Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu ‘UAE’ na mwanaume anayejulikana kwa jina la Sunday Dimonte, Ijumaa linashuka na kilichopatikana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndoa hiyo ilifungwa Juni 17, 2012 na kuhudhuriwa na rafiki wa karibu wa Aunt aliyejulikana kwa jina moja la Rehema bila ndugu, jamaa na marafiki kutoka Bongo.
KISA CHA KUFUNGA NDOA HARAKA
Habari zinadai kuwa, Aunt alifikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kumwambia hawezi kuvumilia umbali uliopo kati ya Tanzania na Dubai hali ambayo Aunt alihofia kupigwa chini.
SHEREHE KUBWA BONGO
Hata hivyo, mpashaji wetu aliweka wazi kuwa baada ya ndoa hiyo, Aunt ameanza maandalizi ya sherehe kubwa Bongo ambapo atawashirikisha mashostito wake.
“Unajua Aunt amefunga ndoa kule bila kuita nduguze kutokana na umbali, lakini atakaporudi Tanzania ataangusha sherehe ya nguvu ambapo sasa, nduguze, jamaa na marafiki wataalikwa,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA AUNT DUBAI
Ijumaa lilimsaka Aunt kwa njia ya simu ya kiganjani akiwa Dubai, alipopatikana na kuulizwa kama kweli amepigwa pingu za maisha, alifunguka:
“Ni kweli nimefunga ndoa huku Dubai lakini nimesikiasikia kuna watu wanasema nilifanya siri. Siyo siri, ila huku ni mbali na huko nyumbani Tanzani, isingekuwa rahisi kuita watu wangu wa karibu.”
Paparazi: Kwa hiyo ndiyo imetoka hiyo?
Aunt: Hapana, nitakaporudi nyumbani nitafanya sherehe, nitaalika watu, hata wewe, tena itabidi unichangie jamani.
WABONGO WANA WASIWASI
Wakati Aunt akikiri kwa kinywa chake kufunga ndoa, baadhi ya Watanzania waliozinyaka taarifa hizo wanadai wana mashaka.
“Mh! Eti jamani, ni kweli Aunt amefunga ndoa Dubai? Mbona siamini. Au kafunga ya kwenye filamu?” alihoji staa mmoja wa filamu aliposikia ishu hiyo.
No comments:
Post a Comment