MREMBO anayeshikilia taji la Miss Kinondoni 2011-12, Stella Mbuge amepigwa ‘stop’ kwenda kumuona mchumba wake Joseph Shamba ‘Vengu’ aliyerudi hivi karibuni akitokea nchini India kwenye matibabu.
Akizungumza na Ijumaa juzikati maeneo ya Leaders Club jijini Dar, Mbuge alisema amekuwa na shauku kubwa ya kwenda kumjulia hali mpenzi wake huyo lakini baadhi ya ndugu wa Vengu wamekuwa wakimzuia kwa madai eti atavujisha siri za mgonjwa.
“Huwezi kuamini tangu Vengu amerudi sijawahi kumuona hata siku moja, nasikia tu mara yuko Kimara mara Mabibo lakini siwezi kwenda kutokana tayari nishachimbwa mkwara na mmoja wa ndugu zake nisikanyage kwao, eti naweza kutoa siri za mgonjwa, sijui ni siri gani hiyo,” alisema mrembo huyo.
Stella na Vengu wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na inadaiwa walikuwa na malengo ya kuja kuoana baadaye lakini kitendo cha miss huyo kutoenda kumjulia hali mwenzake kimekuwa kikiwashangaza wengi.
No comments:
Post a Comment