Thursday, July 26, 2012

YANGA YAITOWA APR

Wachezaji wa Yanga wakiwa wanashangilia ushindi wao walio upata baada ya kuifunga APR,Yanga wasema bdo Azam.

Tuesday, July 24, 2012

KILICHO WAKUTA SIMBA JANA NOMA,WALE LIA MACHOZI YA DAMU

Mnyama auwawa Msitu wa Pande  Send to a friend

Wachezaji wa Azam wakishangilia bao la pili lililofungwa na mshambuliaji John Boko katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Azam ilishinda 3-1. Picha na Michael Matemanga.
MSITU wa Pande ni jina maarufu nchini kwa sasa kutokana na matukio ya watu kutekwa na kupelekwa huko kuteswa na  kuuwawa kinyama.

Kitendo kama hicho cha kinyama ndicho kinachofananishwa na ilichofanyiwa Simba  jana na mshambuliaji wa Azam, John Boko baada ya kufunga mabao matatu pekee na kuiwezesha timu yake kushinda 3-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Kwa ushindi huo sasa Azam itacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DR Congo iliyoitoa Atletico ya Burundi kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa awali.

Boko alifunga bao lake la kwanza dakika 17, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahimu Shikanda, kisha akapachika la pili kwa shuti dakika 46 akimalizia pasi ya Kipre Tchetche, kabla ya Shomari Kapombe kuifuta machozi Simba dakika 53, lakini Boko mfungaji bora wa msimu uliopita alizima ndoto za Simba kurudi kwa kupachika bao la tatu kwa shuti la chini lililomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni.

Katika kile kinachoonekana kujaa kwa imani za kishirikina jana klabu za Simba na Azam hazikutumia mlango mkuu wa kuingilia uwanjani baada ya kumaliza kufanya mazoezi.

Simba wenyewe walitokea geti la kaskazini na Azam walipita mlango tofauti wakati wakirejea vyumbani tayari kujiandaa na mechi hiyo.

Simba ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufika  langoni kwa Azam katika dakika ya kwanza na saba, lakini Haruna Moshi na Felix Sunzu na Uhuru Selemani walishindwa kutumia nafasi hizo.

Katika mechi hiyo Sunzu alipewa kadi ya njano na mwamuzi Issa Kangabo kutoka Rwanda kwa kumchezea vibaya Tchechte.

Mwanzoni mwa kipindi cha kwanza Uhuru Selemani alipoteza nafasi mbili za kufunga baada ya kuwatoka mabeki wa Azam, lakini jitihada zake ziliishia mikononi mwa kipa Deogratius Munishi, huku Azam wakijibu mapigo dakika 14 baada ya Kipre kuwatoka mabeki wa Simba na kupitisha pasi kwa Hamis Mcha aliyepiga fyongo shuti lake.

Dakika ya 17 beki Shikanda wa Azam alipokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na kupiga krosi iliyotua kichwani kwa Bocco ambaye alipiga kichwa kilichokwenda wavuni na kumwacha Kaseja akiwa amesimama.

Simba walijaribu kurudi mchezoni, lakini mashuti ya Kapombe na Mwinyi Kazimoto dakika 34 na 36 yalishindwa kulenga goli. Dakika 41 mwamuzi aliinyima Simba penalti baada ya Kazimoto kumuangusha Ramadhan Chombo kwenye eneo la hatari.

Azam  walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 46 kupitia Boko aliyemalizia vizuri kazi ya Tchetche aliyekuwa mwiba kwa ngome ya Simba.

Mchezaji bora wa mwaka wa Taswa, Kapombe aliifungia Simba bao dakika 53 akipokea krosi ya Haruna Shamte na kupiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lililomshinda Munishi.

Kocha wa Azam, Stewart Hall aliwapumzisha Tchetche, Mcha na kuwaingiza George Odhiambo na Jabir Aziz, wakati Simba ilimtoa Uhuru, Jonas Mkude, Mudde Musa na kuwaingiza Kigi Makasi, Amri Kiemba na Hamis Kinje.

Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na faida kwa Azam kwani dakika 73, Aziz alitoa pasi kwa Boko na kupiga shuti la chini akiwa nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kuwanyamazisha kabisa mashabiki wa Simba.

Awali Atletico ya Burundi inayosifiwa kwa kucheza soka ya kuvutia iliyaaga mashindano hayo kwa kuchapwa mabao 2-1 na AS Vita ya DR Congo.

Mshambuliaji Etekiama Taddy alifunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo alipozifumania nyavu za Atletico katika dakika ya 8 na kuifanya AS Vita kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Atletico ilirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika 48 kwa shuti kali lililopigwa naPierre Kwizera akiitumia vizuri pasi iliyopigwa na Henry Mbazumutima.

Wakati mashabiki wakidhani mpira huo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, mshambuliaji Basilua Makola aliifungia AS Vita bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-1.

Nusu fainali ya michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa Azam kuivaa AS Vita saa nane mchana na mabingwa watetezi Yanga kupepetana na APR saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

kADA WA CCM AFUNGWA JELA KWAJILI YA KULA PESA ZA EPA

 Send to a friend
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka 18 jela Kada wa CCM, Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein katika kesi ya tuhuma za kuchota Sh2.2 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mahakimu wawili katika jopo la waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo waliwatia hatiani watuhumiwa kwa makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo hilo, Jaji Fatuma Masengi aliwaachia huru washtakiwa hao kwa maelezo kwamba upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka yote saba yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo, hukumu hiyo haikuweza kuwaokoa watuhumiwa na hasa Farijala na Maranda watatumikia adhabu yao kwa miaka mitatu jela kwa kuwa adhabu zote walizopewa zitakwenda kwa wakati mmoja.

Tayari Maranda na Farijala wanatumikia kifungo kingine cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za EPA, ambapo walihukumiwa na mahakama hiyo Mei 23, 2011.

Jopo lagawanyika
Jopo la mahakimu watatu lililokuwa likisoma hukumu hiyo liligawanyika na kusoma hukumu mbili tofauti, ambapo hukumu moja iliyoandaliwa na kusomwa na kiongozi wa jopo hilo, Jaji Masengi aliyewaachia huru washtakiwa.

Hata hivyo, katika hukumu ya pili, iliyoandaliwa na Hakimu Projestus Kahyoza na mwenzake Catherine Revocate iliwatia hatiani washtakiwa katika makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili, na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa.

Hata hivyo, wakati wakisoma hukumu hiyo, mahakimu hao walisema badala ya washtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 18, hukumu yao itaenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Kabla ya hukumu
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, hakimu Kahyoza na mwenzake walipitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa  mashtaka  akiwamo mtaalamu wa maandishi, Joseph Mgendi ambaye aliweza kuangalia saini katika nyaraka halisi na zinazodaiwa kughushiwa,  ikiwamo hati ya usajili  ambapo alibainisha kuwa zilikuwa zimeghushiwa.

Pia walipitia utetezi uliotolewa wa mshtakiwa Maranda, ambaye aliyakana mashtaka yote saba yanayowakabili na kwamba, alikataa katakata kuwa hakuwahi kula njama na kughushi hati ya usajili wa Kampuni ya Money Planners & Consultant.

Hakimu Kahyoza alisema, Maranda alidai kuwa yeye hakuwahi kwenda Brela kusajili kampuni hiyo na kwamba, aliyewahi kwenda kusajili kampuni ni binamu yake, Farijala.

Hakimu Kahyoza alisema, Maranda katika utetezi wake alisema yeye hakuwahi kughushi hati yoyote hivyo, haikuwa rahisi kwake kutoa hati iliyoghushiwa pia, hakuwahi kuiba fedha BoT na wala hakuwahi kujipatia fedha yoyote kwa njia ya udanganyifu.

Kahyoza alifafanua kwamba, Maranda alidai mfumo uliotumika kuwaingizia fedha kwenye akaunti yao iliyopo katika Benki ya CBA uliendeshwa kihalali ndiyo maana, BoT hawakuwahi kulalamika hivyo, aliiomba mahakama imuone hana hatia.

Akisoma utetezi uliotelewa na Farijala, Hakimu Kahyoza alisema, Farijala naye alikataa  madai ya kughushi, kuwasilisha nyaraka bandia benki, kuiba fedha yoyote na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na aliiomba mahakama imwachie huru kwa sababu hana hatia.

Yasiyo na utata
Hakimu Kahyoza alisema kuwa mahakama ilibaini kuwapo kwa masuala yasiyokuwa na utata ambayo ni pamoja na kwamba Maranda na Farijala ni ndugu, waliwahi kufanya biashara pamoja na waliingiziwa fedha kwenye akaunti namba 0101379004 ya United Bank of Africa ambazo ni kiasi cha Sh2.2 bilioni.

“Baada ya kuweka msingi huo, mahakama ilijiuliza je, washtakiwa walikula njama ya kuiibia  BoT, walighushi hati ya usajili wa kampuni namba 150731, walighushi hati ya mkataba kati ya Kampuni ya Money Planners & Consultant  na Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani, waliwasilisha nyaraka za kughushi benki, waliibia BoT na kwamba je, walijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,” alihoji Kahyoza.

Hakimu huyo alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa,  hakuna utata kuwa hakuna mahali panapoonyesha washtakiwa ndiyo walikuwa wamiliki wa kwanza wa kampuni hiyo Money Planners & Consultant na kwamba majina yanayodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni  hiyo ya Thobias  Kitunga na Paulo  ni majina ya uongo na ya kufikirika.

Alisema licha ya majina hayo kuwa ya kufikirika, mabadiliko ya kampuni hiyo ya Money Planners & Consultant hayakuwahi kufanyika na hata Brela hakuna kumbukumbu, hivyo saini zilizopo katika nyaraka za kampuni hiyo ikiwamo hati ya usajili ni za kughushi.

Alisema sababu ya kuthibitisha hilo ni kwamba, ofisi ni ileile iliyopo Magomeni Mapipa, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 hata baada ya mabadiliko.

“Hati hizo za usajili hazikusainiwa na Msajili wa Biashara toka Brela, Noel Shani bali zilisainiwa na washtakiwa wenyewe. Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 333 na 335 (c) (e) vimetufanya tufikie hitimisho kuwa  washtakiwa walighushi nyaraka hizo,” alisema Hakimu Kahyoza.

Alisema Maranda na Farijala walighushi hati ya mkataba ya Septemba 8, 2005, wakitumia majina ya Thobiasi na Paul na kwamba hati hiyo haikusainiwa na Kampuni ya Money Planners & Consultant.

“Maombi ya kupewa fedha hizo Sh 2.2 bilioni,  yalipitiwa na watu kadhaa wakiwamo Mwanasheria wa BoT na  kupeleka kibali cha mwisho kwa Gavana aidhinishe malipo, hakuna hata mmoja aliyebaini kuwa katika hati ya mkataba kati ya Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani na Kampuni ya Money Planners & Consultant, haikuwa na saini ya Kampuni ya  Money Planners & Consultant,” alisema.

Aliongeza: “Kwa sababu hiyo inaonyesha wazi, washtakiwa ndiyo walighushi  nyaraka hizo hivyo hati ya usajili  wa kampuni hiyo, hati ya mkataba ni za kughushi.”

“Tuna haki ya kuamini kuwa washtakiwa kwa kujua, walifanya hivyo kwa nia mbaya ya kuwasilisha hati hizo za kughushi CBA na baadaye BoT”, alisema Kahyozi.

Alisema hakuna ubishi kuwa hakuwapo hata shahidi mmoja aliyewahi kuthibitisha kuwa washtakiwa hao waliwahi kuiibia BoT Sh 660,210,000.

“Katika hili hatupo tayari kukubaliana na upande wa mashtaka kwa sababu halijathibitika”.

Aliongeza kwamba, hakuna utata kuwa BoT iliweka kwenye akaunti ya washtakiwa zaidi ya Sh2.2 bilioni na kwamba, kiwango hicho cha fedha kiliwekwa baada ya washtakiwa kuwasilisha hati za kughushi katika benki hiyo kuu ikiwamo hati ya usajili  na hati ya mkataba.

Hakimu alisema kulikuwapo na maofisa wa juu BoT waliotakiwa walithibitishe hilo, lakini, Mwanasheria wa BoT yeye alikuwa anathibitisha uhalali wa hati hiyo ya mkataba ambayo haikusainiwa upande mmoja na Kampuni ya Money Planners kuwa, “Ina nguvu kisheria hivyo, inaweza kutumiwa  na BoT kuhamisha au kuchukua fedha zinazoongelewa  katika maombi ya washtakiwa”.

Alifafanua hakimu, “Mwanasheria alimaanisha kuna watu wengine walithibitisha, sisi kwa mtazamo wetu ni ajabu kwa maofisa  hao hata mmoja hakuwahi kuona katika hati ya mkataba hakuna saini ya Kampuni ya Money Planners.

Tunajiuliza walimezwa katika huu mtego au walipumbazwa? Kama walipumbazwa, upumbazo huo ulikuwa ni wa hali ya juu na kujikuta wote wanaingia kwenye mtego huu.” alisema Hakimu Kahyoza.

Aliongeza kwamba washtakiwa hao walifanya matendo hayo yote kwa nia mbaya na kuwafanya watu wengine, wawe sehemu ya kughushi.

Kuhusu shtaka la kula njama, kwa ujumla maelezo yote yanaonyesha  Maranda na Farijala, walikubaliana  makazi ya ofisi yawe Magomeni, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 ambako ni nyumbani kwao, waliwasiliana, walikutana, walijadiliana  hivyo walitenda kosa la kula njama.

“Sisi hatuna sababu za kusitasita kuwa kweli washtakiwa walikula njama dhidi ya BoT. Ni kweli walikula njama,” alisisitiza Kahyoza.

Jaji Masengi
Kwa upande wake, Jaji Masengi aliwaachia huru washtakiwa wote kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuyathibitisha mashtaka yote saba yanayowakabili.

Jaji Masengi alisema BoT ndiyo wangekuwa walalamikaji wakuu, lakini haikuwahi kulalamika kutoa fedha hizo zinazodaiwa kuibwa na washtakiwa wala Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani.

Kuhusu kughushi, alisema ushahidi uliotolewa haukutosheleza kuthibitisha kosa hilo na kwamba licha ya utetezi kuwa na upungufu lakini hakukuwa na sababu za kuwatia hatiani.

Kabla ya hukumu
Kabla ya kusomwa kwa hukumu ya Hakimu Khayoza na Hakimu Catherine, Wakili wa Serikali, Alapha Msafiri aliiambia mahakama kuwa washtakiwa siyo wakosaji wa mara ya kwanza, wanatumikia kifungo cha miaka  mitano jela katika kesi namba 1161 ya mwaka 2008.

Msafiri aliiomba mahakama itumie kifungu cha 348 na 358 cha Makosa ya Jinai (CPA), kutoa amri Maranda na Farijala walipe fidia au warejeshe kiasi walichojipatia kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Majura Magafu, anayewatetea Maranda na Farijala, alidai kuwa ni kweli washtakiwa walitiwa hatiani  lakini, isiwe kigezo  cha  kuwapa adhabu kali kwa sababu kesi namba 1163 na 1161 zilifunguliwa  siku moja, zinahusu makosa ya aina moja isipokuwa zilipangiwa jopo tofauti.

“Hii ni tofauti na mtu aliyetenda kosa akaachiwa halafu akafanya tena kosa lingine, pia mazingira ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa yalikuwa na utata kwa namna moja au nyingine na kwamba washtakiwa walitenda makosa bila ya kujua kama wanatenda makosa,” aliwatetea wakili huyo na kuongeza:

“Kwa hiyo ni dhahiri, matukio hayo hayakufanyika kwa makusudi kwa asilimia 100, kwa kuwa wao waliamini ni halali lakini baadaye ilibainika kuwa si halai”.

“Waheshimiwa washtakiwa wote wana matatizo ya kiafya, Farijala ana matatizo ya presha ya macho na Maranda ana tatizo la Figo, naomba kama mahakama itaridhia chini ya kifungu cha 38, ina mamlaka ya kuangalia mazingira ya utendwaji wa matukio, hali za watuhumiwa   na kuwaachia kwa masharti maalumu kutokana na afya zao,”alisema Magafu.

Pia aliiomba mahakama itamke wazi wazi kuwa adhabu watakayopewa washtakiwa kama itakuwa ni ya kifungo, inastahili kuanza lini kwa sababu kumekuwapo na utata wa sheria, kuwa ni lazima wamalize kifungo cha awali ndiyo waanze kingine.

Kwa upande wa Hakimu Catherine Revocate, alisema wamejadiliana  kwa kuangalia mazingira ya kesi, afya za washtakiwa  na kwamba ni wakosaji wa mara ya kwanza kwa sababu kesi hiyo inasimama peke yake, katika shtaka la kwanza hadi la saba kasoro shtaka la sita waliloachiwa huru; washtakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kila kosa.

Pia alifafanua kuwa badala ya washtakiwa hao kutumikia kifungo cha miaka 18 katika mashtaka sita yanayowakabili, kifungo hicho kitakwenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

RAIS WA GHANA HAIAGA DUNIA JANA

 Send to a friend
Tuesday, 24 

RAIS wa Ghana, Evans John Atta Mills (68) amefariki Dunia katika hosipitali moja ya kijeshi iliyopo mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.

Mills amekutwa na mauti siku chache tangu aliporejea kutoka Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za mashirika ya habari ya kimataifa zilizotolewa jana jioni zilisema Rais huyo wa tatu wa Ghana aliugua ghafla juzi Jumatatu na alifariki jana mchana baada ya kuzidiwa.

Shirika la Uingereza Reuters lilimnukuu mmoja wa wasadizi wa Rais Mills akisema kuwa rais huyo alikuwa amethibitika kufariki jana mchana.

Habari zaidi zilisema kwa mujibu wa Katiba ya Ghana, Makamu wa Rais
John Dramani Mahama alikuwa akitarajiwa kuapishwa jana usiku kuchukua nafasi ya Mills ili kuongoza taratibu za mazishi ya mtangulizi wake.

Katika siku za karibuni afya ya kiongozi huyo imekuwa ikiripotiwa kuzorota na mwaka huu pekee ameshakwenda Marekani mara tatu kwa ajili ya tiba.
Mara ya mwisho alionekana hadharani nchini Ghana Juni 3 mwaka huu wakati alipokwenda kutemebelea eneo la ajali ya ndege, ziara ambayo ilizua minong’ono kutokana na wanachi kudai kuwa hakuonekana kuwa mwenye siha njema.

Profesa John Evans Fiifi Atta Mills alizaliwa Julai 21, 1944 na aliapishwa kuwa Rais wa Ghana Januari 7, 2009 baada ya kuwa ameshinda uchaguzi dhidi ya mgombea wa kilichokuwa chama tawala Nana Akufo-Addo katika uchaguzi wa 2008.

Monday, July 23, 2012

GARI NDOGO AINA YA TAX LIKIWA LIMEPATA AJALI ASUBUHI NDANI YA SONGEA KARIBIA NA CHUO CHA MATABIBU

 Gari dogo haina ya taxi likiwa limepata ajali karibia na Chuo Utabibu hapa Songea mjini, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa gari mapaka dereva akashindwa kuincotrol gari.Pia baada ya ajali kutokea dereva alishuka na kutoa plate namba ya gari na kukimbia nayo.
 Huu upande wa nyuma huku gari likiwa limenyanyuka tairi juu baada ya kupta ajali hiyo


 Upande wa ubavuni huku kukiwa na damu kidopgo ambayo alijifutia dereva kabla ya kukimbia
 Maeneo ya mbela gari lilikuwa limeingia kwenye msingi amabo upo maalumu kwajili ya kupitisha maji machafu
Plate namba ya gari hilo imetolewa kabaisaa na dereva alikimbia nayo moja kwa moja

Saturday, July 21, 2012

WEMA AVAMIWA NA MAJAMBAZI


SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.
WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo na kuiba vitu mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme ndani ya gari (control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na madirisha (power window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma (side miller).
Vitu vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni ‘makapeti’ ya ndani na vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani ya geti hilo.
WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na uvamizi huo ambao umemfanya kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa akizingatia kuwa tukio hilo limetokea wakati nyumba yake ina walinzi wawili.
“Ni kweli nimeibiwa hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila mazingira ya kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana walinzi wangu wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?” alisema Wema kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea: “Sikuwa na namna kwao, nilikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe utatuzi wa jambo hili sambamba na kuwabananisha walinzi wangu ambao walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini kama geti la kutokea nje lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe. Lakini hili geti ni gumu, mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua masaa matano ambapo kungekuwa kumekucha.”
INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati ya Juni mwaka huu, staa huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, alitangaza kupitia runinga kwamba anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina kila kitu ndani.
Kwa mujibu wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya nyumba hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja wa Wema, Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na samani zake shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.
HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya Jumanne kuzungumzia tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi zilithibitisha Wema kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni majambazi.

MAMA WA KANUMBA ATAFUTA UKWELI KWA MAMA WA LULU



Mama Kanumba, Flora Mtegoa.

Mama Lulu, Lucresia Karugila.

CHOKOCHOKO zimeanza! Huku kesi ya kifo cha mwanaye ikiendelea na Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akisota nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, mama mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Flora Mtegoa amemvaa mama Lulu, Lucresia Karugila, Ijumaa linafunguka.
MANENO MAZITO YA AIBU
Kwenye mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake Kimara-Temboni, Dar es Salaam, mapema Jumanne wiki hii, mama Kanumba alimtolea mama Lulu maneno mazito huku akimshangaa kwa kushindwa kumpa pole na kumfariji tangu mwanaye afikwe na umauti Aprili 7, mwaka huu.
Mama Kanumba alisema anaongea kwa uchungu kwani hakutegemea kama mama Lulu anaweza kuwa kimya mpaka leo hii bila hata kumpa pole wakati matatizo yamewakuta watoto wao wote.
TUPATE SAUTI YA MAMA KANUMBA
Ijumaa: Ili kupata kile alichokisema mzazi huyo mbele ya gazeti hili, tujiunge naye akiwa nyumbani kwake Kimara-Temboni.
Kwako mama Kanumba: Namshangaa sana mama Lulu kwani namuona kama siyo mzazi mwenzangu. Huwezi amini mpaka leo hii hajawahi hata kunipa pole wala kunitumia ujumbe wa watu kunifariji, hivi anategemea mimi nimfuate? Yeye mwanaye yupo hai wangu ndiyo ametangulia. Nimeona niseme kabisa nimpe habari yake.
Ijumaa: Kwani wewe uliwahi kufanya jitihada za kukutana na kufarijiana naye akakataa?
Mama Kanumba: Mama Lulu siyo kabisa. Aliwahi kufuatwa na kuombwa ushirikiano wakati kesi imefunguliwa akakataa.
Ijumaa: Mbona kuna madai kuwa baada ya kifo cha Kanumba upande wa Lulu ulikufuata ukakataa kutoa ushirikiano?
Mama Kanumba: Sijawahi kuongea na mtu yeyote wa upande wa Lulu. Huyo anayedai alikuja kuniomba ushirikiano nikamfukuza ananisingizia kwani simfahamu Lulu na mama yake zaidi ya kuwaona kwenye vyombo vya habari na filamu (Lulu).
Ijumaa: Je, akikufuata utamkubalia aje kukufariji?
Mama Kanumba: Mimi sina nia mbaya na mama Lulu, kibinadamu namuona kakosea kwani kama yeye alikuwa akiogopa, angetuma watu waje kwa niaba yake. Nilidhani alikuwa akiogopa kuja Sinza (Vatican kwa Kanumba) kwa sababu ya waandishi lakini hata nilipohamia huku (Temboni) hajaja. Ukweli ni kwamba akija nitampokea tu ila sidhani kama ipo siku atakuja, nawashangaa hata washauri wake.
Ijumaa: Unaizungumziaje filamu ya Foolish Age ya Lulu ambayo Kanumba aliipeleka Steps?
Mama Kanumba: Ni kweli filamu hiyo ipo Steps, Kanumba ndiye aliipeleka kwa nia ya kumuinua Lulu lakini kabla haijalipwa mauti yakamkuta. Ingekuwa ya Kanumba ningefuatilia.
Baada ya mahojiano hayo, Ijumaa lilitafuta mzani upande wa pili wa mama Lulu ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
TUJIUNGE NA MAMA LULU AKIWA TABATA
Ijumaa: Mama Lulu gazeti la Ijumaa limezungumza na mama Kanumba anakulaumu kwa kushindwa kumfariji baada ya kifo cha mwanaye Kanumba aliyekutwa na umauti akiwa na Lulu. Je, unalizungumziaje suala hili?
Mama Lulu: Eehee unasemaje? Wewe ni nani? Mwandishi? Nimeshawaambia mniache kabisa kwani bila habari ya Lulu na Kanumba hamuuzi?
Ijumaa: Katika maadili ya kazi yetu mtu mmoja akiongea lolote juu ya mwenzake lazima pande zote zisikilizwe hivyo hii ndiyo nafasi yako. Unalizungumziaje suala hilo la mama Kanumba?
Mama Lulu: Sitaki kushauriwa na wewe mwandishi, nina washauri wazuri tu tena ni watu wazima, tafadhali naomba mniache nipumzike.
KIFUATACHO
Bado kesi ya Lulu ni mbichi ambapo itaendelea kuunguruma baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumaliza utata wa umri na jina la Lulu Julai 23, mwaka huu.
KALAMU YA IJUMAA
Wazazi hawa wanapaswa kuwa na staha kwa sababu kila upande una machungu. Kanumba hatunaye na Lulu yupo nyuma ya nondo. Ni vyema wakakaa chini bila kukorogana ili kupunguza machungu waliyonayo.

MHANDO WA TANESCO ASIMAMISHWA KAZI

 

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi William Mhando
MKURUGENZI Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi William Mhando amesimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo kuanzia jana.
Kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi  na kusainiwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, Mhando amesimamishwa kazi pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa  kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Manunuzi Harun Mattambo.
Hata hivyo, Mhando alisema kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC 1) jana kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na kusimamishwa kwake.

Ingawa  taarifa hiyo ya Mboma haikueleza nani anakaimu nafasi iliyoachwa wazi na Mhando, lakini habari tulizopata kutoka vyanzo vyetu ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco zinasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji atakuwa Felschami Mramba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Usambazaji wa Tanesco.

Hatua hiyo imetangazwa jana jijini Dar es Salaam kufuatia  kikao cha dharura cha Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kilichofanyika  Julai 13 mwaka huu, ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco.
Taarifa hiyo fupi imeeleza  kuwa tuhuma dhidi ya Mhandisi Mhando ni nzito hivyo ni vyema zifanyiwe uchunguzi huru na wa kina.
“Hivyo, Bodi  iliazimia pamoja na mambo mengine kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mboma alibainisha bodi yake kufanya kikao kingine cha dharura jana Julai 14, na kuamua kuwasimamisha kazi watendaji hao mara moja ili kupisha uchunguzi huo.
 “Pamoja na uamuzi huo, Bodi imechukua hatua stahiki za kuhakikisha kwamba shughuli za utendaji na uendeshaji wa Tanesco zinaendelea kama kawaida,” imesema taarifa hiyo.
Awali saa 11 jioni jana waandishi wa habari walijazana katika Ofisi ya Wizara ya Nishati na Madini iliyopo Mtaa wa Ohio, ambapo hawakufanikiwa  kuwaona wakurugenzi hao waliokuwa kwenye kikao huku wakitakiwa kuondoka eneo hilo na kusubiri kwa mbali.
Waandishi hao walilazimika kusubiri kwa takriban saa nzima ndipo alipotokea Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini aliyetambuliwa kwa jina la Fadhili Kileo na kugawa nakala ya taarifa ya kikao hicho huku wakurugenzi hao wakipanda magari yao na kuondoka bila ya kuzungumza  na waandishi hao hali iliyowakera waandishi.
 “Jamani naomba mtusamehe sana, hii siyo kawaida yetu, imekuwa ni dharura tu ndiyo maana mnaona wakurugenzi wanaondoka,” alisema Kileo akiwasihi waandishi wa habari waliokuwa wakilalamika.
Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi naye alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akisema kuwa hahusiki.
“Hapana mimi sihusiki, nendeni kwa hao viongozi waliokuwa kwenye kikao,” alisema  Maswi.
Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tanesco kuanzia tarehe 1 Juni, 2010.
Baada ya uteuzi huo, Mhando alisema atahakikisha wateja wote wa Tanesco wanakuwa na mita za Luku.
Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo.
Mhando alichukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Idris Rashid ambaye alimaliza muda wake wa uongozi.
Wasifu wa Mhando
Mhando aliajiriwa na Tanesco mwezi Oktoba mwaka 1987 kama Mhandisi wa Umeme na baadaye alipandishwa na kuwa Mhandisi katika njia za umeme. Mwaka 1990 hadi 1992 aliteuliwa kuwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida.
Mwaka 1992 hadi 1994 alikuwa Meneja wa Mkoa wa Tanesco, Mkoa wa Mbeya. Alipandishwa cheo mwaka 1995 na kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini Magharibi hadi mwaka 1999.
Ana elimu ya Shahada ya Uzamili (Masters) katika masuala ya umeme aliyoipata mjini Havana nchini Cuba mwaka 1987, pamoja na mafunzo mengine aliyoyapata katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kwa muda mrefu Tanesco imekuwa katika matatizo mbalimbali ya kiutendaji na utoaji huduma yaliyosababisha taifa kuingia katika mgawo wa umeme na kudhoofisha maendeleo na ukuaji wa uchumi.

Matatizo hayo ni pamoja na uchakavu wa mitambo ya Tanesco, hujuma za miundombinu na kuingiwa kwa mikataba mibovu.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), kuwa kuna ubadhirifu ndani ya Tanesco  Mei 7, mwaka huu, Mhando alisema ikigundulika kuna ubadhirifu wowote uliofanyika katika shirika hilo kutokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) basi atakuwa tayari kujiuzulu.

Taarifa ya POAC ilisema shirika hilo lilifanya ununuzi wa kati ya Sh300 bilioni hadi Sh600 bilioni lakini Mhando alisema kuwa si kweli.

"Kama nimekosea niko tayari kujiuzulu na mwajiri akiamua kunihamisha sina tatizo na ninawaambia mimi sina miaka miwili kazini na shirika linapata hati safi hilo mwelewe na mliseme," alisema Mhando.

WAKULIMA TUNDURU WAILALAMIKIA SERIKALI KWA KUWEKA MZABUNI MMOJA TU WA KUSAMBAZA PEMBEJEO KWA ZAO LA KOROSHO

Na Joseph Mwambije
Tunduru

Wakulima wa zao la Korosho wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamelalamikia kitendo cha serikali kuweka mzabuni mmoja tu anayesambaza pembejeo kwa wakulima wote wa zao hilo nchini, hali inayosababisha ashindwe kuhudumia maeneo yote kwa uhakika.
 
Wakizungumza mjini Tunduru juzi wakulima hao wakiwemo wanachama wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), walisema kuwa hali hiyo ya kuwa na wakala mmoja imekuwa ikisababisha ucheleweshaji wa pembejeo za ruzuku mapema kulingana na msimu.
 
“Katika wilaya yetu hii zao kubwa tunalotegemea ni korosho, kwa mwaka huu tuliaambiwa sumu ya kuua wadudu aina sulpher itapatikana kwa muda muafaka ambao ni mwezi wa sita miti inapoanza kutoa maua na itauzwa shilingi 12,000 na itaenda kuchukuliwa Mtwara lakini cha kushangaza wakala tunayemtegeme huku alienda mkoani Mtwara na magari yake na kurudi bila sulpher hiyo kwa maelezo kuwa imekwisha,” walisema wakulima hao.
 
Wamesema kuwa kwa sasa wanatumia gharama kubwa kununua sulpher ili kupulizia maua ya korosho yasianguke, badala ya kutumia shilingi 12,000 kununua kwa bei ya ruzuku sumu hiyo sasa wanainunua kwenye maduka ya kawaida kwa shilingi 50,000 gharama ambayo ni kubwa ukilinganisha na bei ya korosho.
 
Bw. Ali Msanjo mkulima mdogo wa Korosho wilaya ya Tunduru ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao wa Vikundi Vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na ambaye pia ni mdau wa bodi ya korosho Tanzania alisema kikao cha Bodi ya Korosho kilichofanyika Tanga kilikubaliana kuwa asilimia 65 ya mauzo ya korosho itarudi Halmashauri ili kuwezesha kupata pembejeo ya ruzuku kwa wakati lakini wakulima wanashanga makubaliano hayo hayajatekelezwa.
 
Naye Bw. Rashidi Masudi mkulima wa Korosho alisema kinachomshangaza kwa sasa ni kuona wakala waliyekuwa wakimtegemea awauzie pembejeo za ruzuku ya Sulpher kwa sasa anauza dawa hiyo ya sulpher kwa bei isiyokuwa ya ruzuku ya shilingi 35,000 tofauti na wafanyabiashara wengine wanaouza kwa Shilingi 50, 000, jambo ambalo linawapa wasiwasi wakulima kwamba huenda kuna mchezo mchafu umefanyika ili kudhulumu haki yao.

 
 Kwa upande wake  Afisa Pembejeo wa wilaya ya Tunduru Bw. Hassan Simba alisema kuwa wakala wa awali aliyekuwa amekabidhiwa jukumu la kusambaza pembejeo hizo aligundulika kuwa ni mdanganyifu na kwamba hatua za kumuondoa zimeshachukuliwa na wakala mpya ameshapatikana.
 
Alisema kwa mwaka huu mfumo umebadilika kwani mwaka jana walikuwa wanatumia watu wa Bodi ya Korosho lakini kwa mwaka huu wanatumia mfuko wa wakulima wa korosho Tanzania na kwa wilaya ya Tunduru walitegemea kupata ruzuku hiyo mwezi wa tano lakini hali haikuwa kama matarajio yao yalivyokuwa.
Afisa pembejeo huyo aliongeza kwa sasa wameamua kufanya juhudi binafsi ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na kwamba kwa kushauriana na Mkuu wa Wilaya wamefanikiwa kupata tani 50 tu toka kwa msambazaji tofauti na yule anayetegemewa na bodi ya korosho. Alisema kiasi hicho cha tano 50 ndicho kinauzwa kwa shilingi 35,000 badala ya Sh.50, 000 baada ya serikali wilayaguzia wakulima gharama.

CHANDARUA KINAPOTUMIKA KAMA WIGO WA BUSTANI

WAKATI Nchi za Ulaya zikiwasaidia Wabongo vyandarua ili kujikinga na Maralia wengine wanavitumia kama wigo wa Bustani kama picha hii inavyoonesha ktika Maeneo ya Mjimwema Manispaa y Songea Mkoani Ruvuma.

WATATU RUVUMA WANUSURIKA AJALINI BAADA YA GARI KUTUMBUKIA MTONI

 Wananchi wakishaa gari iliyoacha njia na kutumbukia katika mto Matarawe.Ktk ajali hiyo watu watatu walijeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.
 Gari hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba mahindi na kufuatia ajali hiyo wananchi wameomba daraja la Matarawe lipanuliwe ili kuwanusuru na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika daraja hilo
 Gari hilo liligonga kingo za daraja na kuingia nazo mtoni.
 Wananchi bado hawaamini kilichotokea kwamba abiria wamenusurika kutokana na ajali yenyewe ilivyokuwa
Hapa wakiwa wamekaribia kabisa gari wakishangaa.

AJALI YA BOTI ZANZIBAR:Gunia liliniokoa

AJALI YA BOTI ZANZIBAR:Gunia liliniokoa  

Bahari ikichafuka kuna mambo
MTAALAMU WA ATOMIKI ASIMULIA ALIVYOELEA BAHARINI KWA SAA NNE BILA KUJUA KUOGOLEAWAKATI jitihada za kuopoa miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama Jumatano wiki hii zikiendelea, walionusurika kwenye ajali hiyo wameeleza jinsi walivyokumbana na zahama, mmoja wao akiwa mkazi wa Micheweni Pemba, Makame Masoud Ali (18), ambaye alisema kilichomsaidia hadi alipookolewa ni kushikilia gunia kwa zaidi ya saa mbili akielea nalo baharini.Mbali na Ali, mwingine ni mfanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Arusha, Salome Mwambinge ambaye alisema: “Kuokoka kwangu ni miujiza ya Mungu.”
Mwambinge ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar alisema: “Sijui kuogelea, lakini nilikaa kwenye maji kwa saa nne. Nilichoka na kukakata tamaa, nikajiachia ili ikiwezekana nife, lakini nashangaa leo hii ni mzima.”
Mtumishi huyo Tume ya Atomiki ambaye alikuwa safarini kuelekea Pemba kikazi, alisema aliokolewa akiwa hajitambui... “Ninachokumbuka ni kwamba waokoaji walinifunga kamba shingoni nikapata maumivu makali, nikapiga kelele wakaniachia, nikatumbukia tena kwenye maji na baadaye walifanikiwa kuniokoa na kuniweka kwenye boti.”
Alisema wakati akiwa katika harakati za kujiokoa, aliwaona watu kadhaa wakiwa wamekufa wakiwamo watoto.
Kwa upande wake, Ali alisema baada ya meli kuzama na yeye kutupwa nje, aliona gunia na kulidaka. Anasema alilishikilia kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kuonwa na vikosi vya uokoaji.
Abiria mwingine mkazi wa Bagamoyo, Hamisa Akida alisema meli hiyo ilizama ghafla na haikuwa rahisi kuwa na maandalizi ya kujiokoa: “Kwa jinsi meli hiyo ilivyozama ghafla haikuwa rahisi kujiokoa, kilichotokea hadi tukaokolewa ni mapenzi ya Mungu,” alisema.
Alisema hali alipookolewa alikuwa ameshakunywa maji mengi na kuishiwa nguvu... “ lakini nashukuru ni mzima.”

Waliopatikana jana
Wakati majeruhi hao wakieleza hayo, jitihada za vikosi vya uokoaji hadi jana zilifanikisha kupatikana kwa miili 68 na kati ya hiyo 16 ilitambuliwa.

Waliotambuliwa ni Husna Ali Hamis (34) na
Kulthum Haji Khamis (34) wote wakazi wa Bagamoyo na Sichana Pandu (45 wa Kilimahewa Zanzibar).

Wengine ni Nadra Maulid Mkubwa (17) wa Chumuni, Zanzibar, Mwanaidi Abdallah Ramadhani (21) wa Morogoro, Zubeda Jumanne Kwagaya (26- Meya),
Idd Masoud Omari (Miezi 7- Tomondo) Riziki Mohamed Idd (21- Fuoni Zanzibar), Mwanaisha Khamis Haji (75) na Amina Shabani Kibega (24) wote wa Jang’ombe, Zanzibar.
Pia wamo Laki Victor Kadoro (28- Mbagala, Dar es Salaam), Damas Leo Mlima (54- Shangani),
Halima Sharifu Abdala (21-Kigamboni, Dar es Salaam), Ali Juma Ali (44- Jang’ombe, Zanzibar),
Raya Ramadhani Hasani (2- Shakani) Mwanaisha Omari Juma (20- Bunju, Dar es Salaam) na Maryam Idd Omari Omari (25) Shakani.

Washindwa kutambua miili

Hali katika Viwanja vya Maisara, wanakohifadhiwa maiti jana kulikuwa na mkanganyiko baada ya wananchi wengi kushindwa kuwaona ndugu zao ambao walikuwa wamesafiri katika meli hiyo wakiwamo raia wa kigeni.
Maiti moja ya raia wa Kenya imetambuliwa na ndugu zao ambao hata hivyo, walisema wamechanganyikiwa kuhusu namna ya kusafirisha mwili kwenda kwao.
Mmoja wa ndugu, John Mumee alisema wameitambua maiti ya ndugu yao aitwaye Martina Masela... “Lakini hatujui tutaisafirisha vipi kwenda Mombasa kwa sababu hatuna fedha, lakini pia hatuelewi tutasafirisha kwa njia gani kwa sababu mashirika ya ndege hayataki kusafirisha maiti.”
Alisema marehemu alikuwa akisafiri na mumewe, Bernard Kalii kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar wakiwa na ndugu mwingine, Mary Kioko ambao bado hawajapatikana.
“Tumepata maiti hiyo moja lakini wenzake wawili bado hatujawapata, hatuelewi tufanye nini hapa tumechanganyikiwa tunaomba msaada wa haraka,” alisema Mumee.
Waliiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwasiliana na Ubalozi wa Kenya nchini ili kuona kama kuna uwezekano wa kuwasaidia kuisafirisha maiti hiyo ambayo alisema imeanza kuharibika.
Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Ali Mzee Moto alisema, hadi sasa hajawaona binti yake, Mwamini Ali aliyekuwa na mtoto wake mchanga.
“Walisafiri na meli hiyo na walikuwa wakipitia Zanzibar ili siku inayofuata waende Pemba. Alikuwa anamfuata mchumba wake lakini Mungu hakupenda afike huko,” alisema Moto.
Alishangazwa na shughuli ya uokoaji kusuasua na kuhoji sababu za Serikali kushindwa kuomba msaada wa waokoaji kutoka nje.
“Tunafahamu ndugu zetu watakuwa wamekufa, lakini tunachoomba sisi ni kupata miili yao ili twende tukawazike,” alisema Moto.
Mwingine aliyepotelewa na mtoto ni Philip Cassian John anayefanya kazi Trans Cargo, Dar es Salaam alisema, hajamwona mwanaye Thobias Joseph, anayefanya kazi katika Kampuni ya Hugo Domingo aliyesafiri na meli hiyo kwa safari za kikazi.
“Walisafiri na wafanyakazi wenzake ambao maiti zao zimepatikana, sasa niko hapa kusubiri kati ya watakaookolewa leo kama nitamwona mwanangu.”

Maiti zaharibika
Kati ya maiti 68 zilizoopolewa baharini, 10 hazikutambuliwa na zilizikwa jana na SMZ katika makaburi ya Kama huko Bububu, Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mazishi, Abdallah Twalib alisema maiti zimeharibika vibaya.
“Hata baadhi ya ndugu waliozitambua maiti zao wameiomba Serikali izike kwenye makaburi ya eneo la Kama baada ya kuharibika vibaya,” alisema.

Sijiuzulu ng’o

Juzi, Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad alisema hawezi kujiuzulu kwa tukio hilo kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu.
Hamad alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na mawaziri wenzake wanne kutoka katika Serikali ya Muungano na wa SMZ. Hao walikuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Ali Mbarouk na Waziri wa Katiba na Sheria SMZ, Aboubakar Hamis.
Alipoulizwa kama ana mpango wa kujiuzulu kutokana na ajali hiyo ambayo ni ya pili kutokea katika kipindi cha mwaka mmoja, Hamad alisema: “Hivi ningezuiaje upepo usitokee?
Ajali hii ni mapenzi ya Mungu kwani haiwezi kuzuiliwa na binadamu kwa sababu imetokana na upepo mkali na ilitokea ghafla, katika kipindi kisichozidi dakika tano meli ilikuwa imezama,” alisema Hamad.
“Kujiuzulu siyo utatuzi wa tatizo, bali ni kumwomba Mungu atuepushe na majanga kama haya ambayo hayawezi kuzuiwa na binadamu.”
Waziri huyo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa anayetokea Chama cha CUF alisema, kauli za kumtaka ajiuzulu ni mbinu chafu za kisiasa zinazofanywa dhidi yake ili aonekane hafai kuongoza.
“Walinipiga vita hata kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islander wakitaka nijiuzulu lakini hata majibu ya tume iliyoundwa kuchunguza ilinisafisha kwamba sihusiki,” alisema.
Dk Mwakyembe alisema Watanzania hawana sababu ya kumtafuta mchawi wa ajali hiyo kwani imetokea kwa bahati mbaya... “Tukubali kwamba ajali hii ni bahati mbaya. Maofisa wetu wametuthibitishia bila kuwa na shaka kwamba meli ilikuwa nzima na haikuzidisha abiria, kujiuzulu siyo suluhisho, tushikamane katika kipindi hiki kigumu.”

Uzoefu wa mabaharia
Mmoja wa mabaharia katika Kivuko cha Bandari ya Dar es Salaam, John Peter amesema Serikali inapaswa kulaumiwa kwa tukio hilo.
Peter ambaye amekuwa baharia kwa miaka 24 sasa alisema, pamoja na Serikali kuwa na wataalamu wa kukagua vyombo hivyo kabla, ufisadi katika usajili wa meli bado ni tatizo.
“Kama Marine Suveyer (Mtafiti wa Meli) angetekeleza majukumu yake, naamini tusingekuwa na meli mbovu kama hizi,” alisema.
Baharia mwingine mwenye uzoefu wa miaka 40, maarufu kama Kepteni Magamba alisema anayepaswa kulaumiwa katika ajali hiyo ni kiongozi wa safari za meli.
Kiongozi huyo (Port State Controller) hupokea taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa na kuruhusu meli iondoke au isiondoke. Kiongozi huyo husimamia usalama wa meli ndani na nje ya bahari kwa kushirikiana na eneo meli inapoelekea.
“Meli kabla ya kuondoka lazima ifuate taratibu zote, nahodha hupata kibali kutoka Sumatra (clearance) na kuipeleka kwa ‘Port State Controller’ ambaye tayari anakuwa ameshapata taarifa za hali ya hewa,” alisema Magamba.

Wanasiasa

Vyama kadhaa vya siasa vimetoa salamu za pole kwa wafiwa na kuishauri Serikali kuongeza umakini katika ukaguzi wa vyombo vya baharini.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliitaka Serikali kuangalia upya uwajibikaji, utendaji na mwenendo wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) akidai kuwa taasisi hiyo imeshindwa kuwajibika ipasavyo kudhibiti vyombo vya usafiri.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ameshauri kanuni za Bunge zinazotumika hivi sasa kuangaliwa upya ili kuruhusu Bunge kujadili ajali hiyo... “Nimesikitishwa na kitendo cha Naibu Spika (Job Ndugai) kuzuia wabunge kujadili suala la kuzama kwa meli bungeni kwa maelezo kuwa kanuni haziruhusu. Nitoe wito kwa kanuni kuangaliwa upya ili kuruhusu Bunge kujadili masuala ya kitaifa pindi yanapotokea.”
Mwenyekiti wa APPT Maendeleo, Peter Mziray alisema: “Lipo tatizo katika uingizaji, ukaguzi na usajili wa vyombo vya usafirishaji wa majini… Serikali na mamlaka zinazohusika na usajili hazifanyi kazi kwa kuzingatia umuhimu wa kazi waliyopewa na matokeo yake ndiyo kuruhusu vyombo vibovu kubeba roho za watu.”
Sumatra yajitetea
Hata hivyo, Sumatra imejitetea kwamba haitambui usajili wa boti hiyo ya Mv Skagit. Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema meli hiyo ilisajiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Majini Zanzibar (ZMA).
Alisema meli hiyo ilipewa cheti cha ubora na mamlaka hiyo Agosti, 24 mwaka jana ambacho kinamalizika muda wake, Agosti 23, mwaka huu ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 300 na tani 26 za mizigo... “Hatuwezi kutoa maelezo zaidi kwa sababu ilisajiliwa Zanzibar na si huku kwetu.”
Habari hii imeandikwa na Burhani Yakub, Pangani; Raymond Kaminyoge na Salma Said, Zanzibar; Kelvin Matandiko, Nora Damian, Joyce Mmasi, Geofrey Nyang’oro na Aidan Mhando Dar.

MAJENGO MAPYA YAPENDEZESHA TASWIRA YA MJI WA SONGEA

 Majengo mapya yanazidi kupendezesha taswira ya Mji wa Songea ,pichani ni jengo la Ofisi za Hazina Mkoa wa Ruvuma.
Jengo la Watawa Wabenediktine wa Hanga ambalo ujenzi wake unaendelea.

MCHUMBA WA VENGU HAZUIWA KWENDA KUMUONA MPENZI WAKE


Miss Kinondoni 2011-12, Stella Mbuge.
Joseph Shamba ‘Vengu’.

MREMBO anayeshikilia taji la Miss Kinondoni 2011-12, Stella Mbuge amepigwa ‘stop’ kwenda kumuona mchumba wake Joseph Shamba ‘Vengu’ aliyerudi hivi karibuni akitokea nchini India kwenye matibabu.
Akizungumza na Ijumaa juzikati maeneo ya Leaders Club jijini Dar, Mbuge alisema amekuwa na shauku kubwa ya kwenda kumjulia hali mpenzi wake huyo lakini baadhi ya ndugu wa Vengu wamekuwa wakimzuia kwa madai eti atavujisha siri za mgonjwa.
“Huwezi kuamini tangu Vengu amerudi sijawahi kumuona hata siku moja, nasikia tu mara yuko Kimara mara Mabibo lakini siwezi kwenda kutokana tayari nishachimbwa mkwara na mmoja wa ndugu zake nisikanyage kwao, eti naweza kutoa siri za mgonjwa, sijui ni siri gani hiyo,” alisema mrembo huyo.
Stella na Vengu wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na inadaiwa walikuwa na malengo ya kuja kuoana baadaye lakini kitendo cha miss huyo kutoenda kumjulia hali mwenzake kimekuwa kikiwashangaza wengi.

Friday, July 20, 2012


Friday, July 20, 2012

MENEJA WA MELI ILIYOZAMA ZANZIBAR AKAMATWA

Meneja meli iliyozama Zanzibar akamatwa  
FIKIWA WATU 63, SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU MAOMBOLEZO
Wananchi wakiwa kwenye foleni katika viwanja vya Maisara mjini unguja Zanzibar jana kwa ajili ya kwenda kutambua miili ya ndugu zao waliofariki kwenye ajali ya meli MV Skygat, iliyozama eneo la chumbe Zanzibar juzi.
 
 JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

“Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza;

“Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema.


Maiti zilizotambuliwa

Hadi saa 10 jioni jana, maiti 63 zilikuwa zimepatikana na watu 145 kuokolewa wakiwa hai. Hata hivyo kati ya maiti hizo zilizopatikana, matiti 34 zilichukuliwa na ndugu zao.

Baadhi ya maiti waliotambuliwa pamoja na umri wao na maeneo wanayoishi katika mabano ni Anita Emanuel (42,  Kibamba -Dar es Salaam), Rukiya Issa Muombwa (miezi 2, Meli nne –Fuoni Zanzibar ), Halima Ali Khamis (23, Mtopepo- Zanzibar), Kolin Krispin (miezi 9, Kunduchi - Dares Salaam) na Rahma Ali Abdalla (miaka 52, Mfenesini - Zanzibar).

Maiti wengine ni  Said Jumanne Masanja (miaka 9, Nzega Tabora), Sauda Abdalla Omar (22, Ole Pemba), Said Juma Said (36, Arusha),  Amina Abdalla Tindwa, (miezi 6, Fuoni), Halima Ramadhani Kilimo, (53, Morogoro), Khadija Omar Ali (58), Amina Hamir Bakari (39, Chukwani - Zanzibar), Mwanahamisi Mshauri (42, Kibandamaiti),  Ali Hamdu Othman (35, Mkwajuni) na Mohamed Said Salum (40, Magomeni Mikumi - Dares Salaam).

Wengine ni Amina Ahmed Ramadhani (21, Michenzani zanzibar ), Mgeni Juma Halfani (25, Daraja Bovu), Khadija Rajab Kibune (22, Fuoni), Maua Ramadhani Feruzi (29, Mwembeladu), Hussein Ali Khamis (4, Mwanakwerekwe) na Sabiha Heri Mbarouk (25, Mgeleme, Chakechake-Pemba).

Pia wamo Halima Ali Mohamed (35, Kiwengwa- Zanzibar), Asia Juma Khamis (29, Kiembe Samaki), Yusuf Hasan Yusuf (7, Chamanzi, Dar es Salaam), Batuli Abrahmani Amir (20, Jang'ombe), Fatma Said Sultani (54, Msasani Dar es Salaam), Juma Jafari Shajak (Miezi 6, Kimaneta - Tanga) na Mohamed Ali Ngombe (41, Buguruni - Dares Salaam).

Serikali yatangaza siku
tatu za maombolezo

Kufuatia msiba huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 mwaka huu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na shughuli zote zinazoambatana na sherehe na burudani zimefutwa kwa muda huo lakini kazi na shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida

Nayo Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ilitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba huo mkubwa uliolikumba taifa.

Lukuvi aliwaambia waandishi katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zitapepea nusu mlingoti na shughuli za starehe zitasimamishwa ila kazi zitaendelea kama kawaida.

Rais Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu. Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa  ni kuokoa maisha ya watu,” alisema Rais Dk Shein.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa Bungeni Mkoa wa Dar es Salaam ndio umepewa jukumu la kushuhulikia suala hilo.

Alisema kwa sasa mkoa Umepanga kutoa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhi mili ya watu waliofariki katika ajali hiyo.

“Tumepanga kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili ndio itahusika katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo,” alisema Sadick na kuongeza;

“Watu wote ambao wanajua kuwa ndugu zao walisafiri na meli hiyo wafike katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya utambuzi,” alisema na kuongeza kuwa ambayo haitatambuliwa Serikali itachukua jukumu la kuizika.

EU yatoa ndege ya uokoaji

Katika kuonyesha kuguswa na ajali hiyo, Umoja wa Ulaya (EU) umetoa ndege maalum kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji katika eneo la ajali.

Balozi wa Uingereza hapa nchini  Diane Corner aliwaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar kuwa wameamua kutoa msaada wa ndege hiyo ambayo iliwasaili Zanzibar usiku wa kuamkia Julai 19, kitokea katika visiwa vya Ushelisheli.

“Hii ni ndege maalum ambayo kazi yake ni kuratibu na kubainisha eneo ambalo kuna watu na inawasiliana na waokoaji walioko majini ikiwa angani,” alisema Balozi Corner.

Alifafanua kwamba, Umoja wa Ulaya unaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  katika kazi ya uokoaji, lakini pia Umoja huo upo tayari kutoa msaada wowote utaohitajika.

Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Leahant Alfonso alisema Serikali yake imetoa msaada wa dawa kwa ajili ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Balozi Alfonso aliipongeza SMZ kwa kuchukua hatua haraka kukabiliana na maafa hayo.

“Nawapa pole watu wa Zanzibar kwa msiba huu, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana, hasa nilipoziona maiti saba za watoto wadogo. Moyo wangu umeumia sana,” alisema huku akibubujikwa machozi.

Wabunge wachangia maafa
 
Katika hatua nyingine, wabunge wote watakatwa posho ya siku moja kuchangia maafa ya kuzama kwa boti  hiyo huku  Bunge likiahirishwa kwa siku moja kuomboleza maafa hayo.

Posho hizo za wabunge zitawezesha kupatikana kwa Sh24.6 milioni kutoka kwa Wabunge wa sasa 352 ambao kila mmoja atachagia Sh70,000.

Spika Anne Makinda jana asubuhi aliahirisha shughuli za Bunge kwa siku moja na kutangaza kuwa, Kamati ya Uongozi ya Bunge katika kikao chake jana asubuhi, iliamua zikatwe posho za siku moja na fedha hizo zitatolewa kama rambirambi kwa ndugu wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.



Wakizungumza baada ya ajali hiyo, baadhi ya wabunge waliitupia lawama Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kwa kile walichodai kuwa ilishindwa kutoa taarifa ya tahadhari kwa watumiaji wa usafiri wa majini.

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema mamlaka hiyo inabeba lawama kwa kushindwa kutoa ushauri kwa vyombo husika na badala yake wanafanya kazi ya kutabiri mvua tu.

“Wale jamaa hawafai kabisa, matatizo yote wanatakiwa kubebeshwa wao kwa kuwa hawakuweza kutoa ushauri juu ya nini kingetokea mbele ya safari,’’ alisema Lusinde.

Mbali na Mamlaka ya Hali ya hewa, lakini mbunge huyo alitaka pia wakaguzi wa vyombo vya majini kuwajibika kwa kushindwa kukagua uimara wa vyombo hivyo.


Kwa upande wake Mbuge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata alisema tukio la kuzama kwa meli hiyo alilipokea kwa masikitiko lakini akasema “ni kazi ya Mungu.’’

Mlata alisema tangu juzi yeye pamoja na wabunge wengine wako katika maombi mazito ya kutaka Mungu awanusuru majeruhi na kuwapa nguvu ya ujasiri waokoaji ili wafanya kazi yao kwa moyo wa kujituma zaidi.

“Unajua tunafanya mambo tangu tulipopata taarifa za ajali hiyo na hadi sasa tunatakiwa kuendelea kufanya maombi hayo kwa ajili yha ndugu zetu, naamini mkono wa Mungu hautapungukia kitu,’’alisema Mlata.


Ushuhuda wa mabaharia, waokoaji

Akizungumzia  ajali hiyo, mmoja wa waokoajii binafsi, waliofika katika tukio hilo alisema boti hiyo imebinuka ikiwa mgongo juu.

Mmoja wa wahanga aliyenusurika katika ajali hiyo, Hassan Khatib alisema tangu waliondoka Dar es Salaam mnamo  saa 6:00 mchana juzi, hali ya bahari ilikuwa mbaya kwa sababu kulikuwa na mawimbi makubwa baadaye meli ilizidiwa na kupoteza mwelekeo.

Alisema baada ya hapo ililala upande na kisha ilibinuka na yeye kutupwa kwenye maji na akawa hana kitu cha kushika ndipo alianza kuogelea na kufanikiwa kushi ubao na kuogelea nao.

Alisema huduma uokoaji zilichelewa kufika ila mara baada ya ajali ilifika ndege na kuzunguka katika eneo la tukio na kuondoka na baada ya  saa kadhaa vilifika vyombo ukoaji.

TMA watoa kauli
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Hamza Kabelwa alisema kuwa, kupitia ofisi yao iliyopo bandarini Dar es Salaam walitoa taarifa kwenye vyombo vya usafiri wa majini juu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini kwa kasi ya kilometa tatu kwa saa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi.
“Tulipogundua hali hiyo tulitoa taarifa kwa wahusika wa vyombo vya usafiri wa majini tu,” alifafanua Dk Kabelwa.
Meli ya Skagit ilitengenezwa mwaka 1989 nchini Marekani na ilikuja nchini 2008.
Shahihisho
Jana gazeti hili lilichapisha kwa makosa kuwa meli iliyozama inaitwa MvSkad badala ya Skagit.

Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Habiel Chidawali, Dodoma, Salma Said, Zanzibar
Aidan Mhando, Pamela Chilongola na Victoria Mhagama, Dar

KUTANA NA BINGWA WA KUCHEKA TANZANIA

 Hapa anatafakri jambo  ni namna gani atapata Mtu wa kushindana nae,maana wengi wanamkimbia hata Masudi Sura mbaya alimkimbia kwenye shindano la kumtafuta mwenye sura mbaya Tanzania.
Huyu ni Msanii Bingwa wa kucheka Tanzani na duniani kwa ujumla ambapo ana uwezo wa kucheka kwa dakika 18 bila kupumzika hapa alikuwa akipafomu kabla Waziri Mkuu Mizengo Pinda hajapand jukwaani kuhutubia Wananchi Mkoani ruvuma hivi Karibuni.

WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA KIKATILI MTOTO WAO MCHANGA KWA KUMNYONGA

WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA KIKATILI MTOTO WAO MCHANGA KWA KUMNYONGA
Na Joseph Mwambije,
Songea

MHANDO WA TANESCO AICHANGANYA SERIKALI NA WABUNGE

 
Mkurugenzi Mkuu wa shirika Tanesco,William Mhando
FHATUA ya Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando imeibua mvutano kati ya wabunge na Serikali.
Mwishoni mwa wiki, bodi hiyo iliwasimamisha kazi Mhando, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Huduma za Tanesco, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Ununuzi,  Harun Mattambo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walio katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na wengine wa Kamati ya Nishati na Madini, wamesema uamuzi huo umejaa maswali kuliko majibu.

Moja ya maswali hayo ni mchakato wa kumsimamisha wakihoji kikao kilichochukua uamuzi huo kuitishwa na wizara badala ya bodi, kupatikana Mkaguzi Kampuni ya Ernst&Young kukagua hesabu za Tanesco bila kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma na tuhuma za ukabila dhidi ya bosi huyo wa Tanesco.

Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo  za wizara kuingilia mamlaka ya bodi, alijibu: “Kesho (leo) tunakutana na kamati, kwa hiyo siwezi kuzungumza chochote nitazungumza ndani ya kamati.”

Hata hivyo, habari kutoka kamati hizo za Bunge zinasema mkutano kati ya watendaji wa wizara, bodi na wajumbe wa kamati hizo unatarajiwa kuwa na mvutano mkali.

Tayari baadhi ya wajumbe wa POAC wamehoji tuhuma za ukabila ambazo anatuhumiwa kuwa nazo Mhando, huku wakimnyooshea kidole Maswi na waziri wake.

“Hivi Mhando ukabila wake ni nini...? Hivi, tunapaswa kujadili uwezo wa mtu au kabila lake?” alihoji mmoja wa wajumbe wa POAC.

Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alipoulizwa kuhusu kikao chao cha kesho alisema tayari wameshamwandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na wanatarajia kukutana na bodi kupata ufafanuzi.

Kusimamishwa Mhando
Hatua hiyo ya kumsimamisha Mhando ilitangazwa mwishoni mwa wiki na bodi hiyo baada ya kikao cha dharura ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma na kuchukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Hivyo, Bodi iliazimia pamoja na mambo mengine, kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,” ilieleza sehemu ya taarifa aliyoitoa Mboma kwa vyombo vya habari.

Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Juni Mosi, 2010 akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Dk Idris Rashidi ambaye alimaliza muda wake wa uongozi.

Mara baada ya uteuzi huo, Mhando alisema kwamba moja ya mambo ambayo atahakikisha anayatekeleza ni kuhakikisha kuwa wateja wote wa shirika hilo wanakuwa na mita za Luku.

Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo.

AJALI YA MELI ILITISHAKWELI


 
FIKIWA WATU 63, SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU MAOMBOLEZO
Wananchi wakiwa kwenye foleni katika viwanja vya Maisara mjini unguja Zanzibar jana kwa ajili ya kwenda kutambua miili ya ndugu zao waliofariki kwenye ajali ya meli MV Skygat, iliyozama eneo la chumbe Zanzibar juzi.
 
 JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

“Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza;

“Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema.


Maiti zilizotambuliwa

Hadi saa 10 jioni jana, maiti 63 zilikuwa zimepatikana na watu 145 kuokolewa wakiwa hai. Hata hivyo kati ya maiti hizo zilizopatikana, matiti 34 zilichukuliwa na ndugu zao.

Baadhi ya maiti waliotambuliwa pamoja na umri wao na maeneo wanayoishi katika mabano ni Anita Emanuel (42,  Kibamba -Dar es Salaam), Rukiya Issa Muombwa (miezi 2, Meli nne –Fuoni Zanzibar ), Halima Ali Khamis (23, Mtopepo- Zanzibar), Kolin Krispin (miezi 9, Kunduchi - Dares Salaam) na Rahma Ali Abdalla (miaka 52, Mfenesini - Zanzibar).

Maiti wengine ni  Said Jumanne Masanja (miaka 9, Nzega Tabora), Sauda Abdalla Omar (22, Ole Pemba), Said Juma Said (36, Arusha),  Amina Abdalla Tindwa, (miezi 6, Fuoni), Halima Ramadhani Kilimo, (53, Morogoro), Khadija Omar Ali (58), Amina Hamir Bakari (39, Chukwani - Zanzibar), Mwanahamisi Mshauri (42, Kibandamaiti),  Ali Hamdu Othman (35, Mkwajuni) na Mohamed Said Salum (40, Magomeni Mikumi - Dares Salaam).

Wengine ni Amina Ahmed Ramadhani (21, Michenzani zanzibar ), Mgeni Juma Halfani (25, Daraja Bovu), Khadija Rajab Kibune (22, Fuoni), Maua Ramadhani Feruzi (29, Mwembeladu), Hussein Ali Khamis (4, Mwanakwerekwe) na Sabiha Heri Mbarouk (25, Mgeleme, Chakechake-Pemba).

Pia wamo Halima Ali Mohamed (35, Kiwengwa- Zanzibar), Asia Juma Khamis (29, Kiembe Samaki), Yusuf Hasan Yusuf (7, Chamanzi, Dar es Salaam), Batuli Abrahmani Amir (20, Jang'ombe), Fatma Said Sultani (54, Msasani Dar es Salaam), Juma Jafari Shajak (Miezi 6, Kimaneta - Tanga) na Mohamed Ali Ngombe (41, Buguruni - Dares Salaam).

Serikali yatangaza siku
tatu za maombolezo

Kufuatia msiba huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 mwaka huu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na shughuli zote zinazoambatana na sherehe na burudani zimefutwa kwa muda huo lakini kazi na shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida

Nayo Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ilitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba huo mkubwa uliolikumba taifa.

Lukuvi aliwaambia waandishi katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zitapepea nusu mlingoti na shughuli za starehe zitasimamishwa ila kazi zitaendelea kama kawaida.

Rais Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu. Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa  ni kuokoa maisha ya watu,” alisema Rais Dk Shein.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa Bungeni Mkoa wa Dar es Salaam ndio umepewa jukumu la kushuhulikia suala hilo.

Alisema kwa sasa mkoa Umepanga kutoa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhi mili ya watu waliofariki katika ajali hiyo.

“Tumepanga kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili ndio itahusika katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo,” alisema Sadick na kuongeza;

“Watu wote ambao wanajua kuwa ndugu zao walisafiri na meli hiyo wafike katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya utambuzi,” alisema na kuongeza kuwa ambayo haitatambuliwa Serikali itachukua jukumu la kuizika.

EU yatoa ndege ya uokoaji

Katika kuonyesha kuguswa na ajali hiyo, Umoja wa Ulaya (EU) umetoa ndege maalum kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji katika eneo la ajali.

Balozi wa Uingereza hapa nchini  Diane Corner aliwaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar kuwa wameamua kutoa msaada wa ndege hiyo ambayo iliwasaili Zanzibar usiku wa kuamkia Julai 19, kitokea katika visiwa vya Ushelisheli.

“Hii ni ndege maalum ambayo kazi yake ni kuratibu na kubainisha eneo ambalo kuna watu na inawasiliana na waokoaji walioko majini ikiwa angani,” alisema Balozi Corner.

Alifafanua kwamba, Umoja wa Ulaya unaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  katika kazi ya uokoaji, lakini pia Umoja huo upo tayari kutoa msaada wowote utaohitajika.

Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Leahant Alfonso alisema Serikali yake imetoa msaada wa dawa kwa ajili ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Balozi Alfonso aliipongeza SMZ kwa kuchukua hatua haraka kukabiliana na maafa hayo.

“Nawapa pole watu wa Zanzibar kwa msiba huu, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana, hasa nilipoziona maiti saba za watoto wadogo. Moyo wangu umeumia sana,” alisema huku akibubujikwa machozi.

Wabunge wachangia maafa
 
Katika hatua nyingine, wabunge wote watakatwa posho ya siku moja kuchangia maafa ya kuzama kwa boti  hiyo huku  Bunge likiahirishwa kwa siku moja kuomboleza maafa hayo.

Posho hizo za wabunge zitawezesha kupatikana kwa Sh24.6 milioni kutoka kwa Wabunge wa sasa 352 ambao kila mmoja atachagia Sh70,000.

Spika Anne Makinda jana asubuhi aliahirisha shughuli za Bunge kwa siku moja na kutangaza kuwa, Kamati ya Uongozi ya Bunge katika kikao chake jana asubuhi, iliamua zikatwe posho za siku moja na fedha hizo zitatolewa kama rambirambi kwa ndugu wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.



Wakizungumza baada ya ajali hiyo, baadhi ya wabunge waliitupia lawama Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kwa kile walichodai kuwa ilishindwa kutoa taarifa ya tahadhari kwa watumiaji wa usafiri wa majini.

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema mamlaka hiyo inabeba lawama kwa kushindwa kutoa ushauri kwa vyombo husika na badala yake wanafanya kazi ya kutabiri mvua tu.

“Wale jamaa hawafai kabisa, matatizo yote wanatakiwa kubebeshwa wao kwa kuwa hawakuweza kutoa ushauri juu ya nini kingetokea mbele ya safari,’’ alisema Lusinde.

Mbali na Mamlaka ya Hali ya hewa, lakini mbunge huyo alitaka pia wakaguzi wa vyombo vya majini kuwajibika kwa kushindwa kukagua uimara wa vyombo hivyo.


Kwa upande wake Mbuge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata alisema tukio la kuzama kwa meli hiyo alilipokea kwa masikitiko lakini akasema “ni kazi ya Mungu.’’

Mlata alisema tangu juzi yeye pamoja na wabunge wengine wako katika maombi mazito ya kutaka Mungu awanusuru majeruhi na kuwapa nguvu ya ujasiri waokoaji ili wafanya kazi yao kwa moyo wa kujituma zaidi.

“Unajua tunafanya mambo tangu tulipopata taarifa za ajali hiyo na hadi sasa tunatakiwa kuendelea kufanya maombi hayo kwa ajili yha ndugu zetu, naamini mkono wa Mungu hautapungukia kitu,’’alisema Mlata.


Ushuhuda wa mabaharia, waokoaji

Akizungumzia  ajali hiyo, mmoja wa waokoajii binafsi, waliofika katika tukio hilo alisema boti hiyo imebinuka ikiwa mgongo juu.

Mmoja wa wahanga aliyenusurika katika ajali hiyo, Hassan Khatib alisema tangu waliondoka Dar es Salaam mnamo  saa 6:00 mchana juzi, hali ya bahari ilikuwa mbaya kwa sababu kulikuwa na mawimbi makubwa baadaye meli ilizidiwa na kupoteza mwelekeo.

Alisema baada ya hapo ililala upande na kisha ilibinuka na yeye kutupwa kwenye maji na akawa hana kitu cha kushika ndipo alianza kuogelea na kufanikiwa kushi ubao na kuogelea nao.

Alisema huduma uokoaji zilichelewa kufika ila mara baada ya ajali ilifika ndege na kuzunguka katika eneo la tukio na kuondoka na baada ya  saa kadhaa vilifika vyombo ukoaji.

TMA watoa kauli
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Hamza Kabelwa alisema kuwa, kupitia ofisi yao iliyopo bandarini Dar es Salaam walitoa taarifa kwenye vyombo vya usafiri wa majini juu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini kwa kasi ya kilometa tatu kwa saa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi.
“Tulipogundua hali hiyo tulitoa taarifa kwa wahusika wa vyombo vya usafiri wa majini tu,” alifafanua Dk Kabelwa.
Meli ya Skagit ilitengenezwa mwaka 1989 nchini Marekani na ilikuja nchini 2008.
Shahihisho
Jana gazeti hili lilichapisha kwa makosa kuwa meli iliyozama inaitwa MvSkad badala ya Skagit.

Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Habiel Chidawali, Dodoma, Salma Said, Zanzibar
Aidan Mhando, Pamela Chilongola na Victoria Mhagama, Dar