WAJANJA WA TOWN
Saturday, March 16, 2013
Thursday, July 26, 2012
Tuesday, July 24, 2012
KILICHO WAKUTA SIMBA JANA NOMA,WALE LIA MACHOZI YA DAMU
Mnyama auwawa Msitu wa Pande | Send to a friend |
Kitendo kama hicho cha kinyama ndicho kinachofananishwa na ilichofanyiwa Simba jana na mshambuliaji wa Azam, John Boko baada ya kufunga mabao matatu pekee na kuiwezesha timu yake kushinda 3-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo sasa Azam itacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DR Congo iliyoitoa Atletico ya Burundi kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa awali. Boko alifunga bao lake la kwanza dakika 17, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahimu Shikanda, kisha akapachika la pili kwa shuti dakika 46 akimalizia pasi ya Kipre Tchetche, kabla ya Shomari Kapombe kuifuta machozi Simba dakika 53, lakini Boko mfungaji bora wa msimu uliopita alizima ndoto za Simba kurudi kwa kupachika bao la tatu kwa shuti la chini lililomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni. Katika kile kinachoonekana kujaa kwa imani za kishirikina jana klabu za Simba na Azam hazikutumia mlango mkuu wa kuingilia uwanjani baada ya kumaliza kufanya mazoezi. Simba wenyewe walitokea geti la kaskazini na Azam walipita mlango tofauti wakati wakirejea vyumbani tayari kujiandaa na mechi hiyo. Simba ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufika langoni kwa Azam katika dakika ya kwanza na saba, lakini Haruna Moshi na Felix Sunzu na Uhuru Selemani walishindwa kutumia nafasi hizo. Katika mechi hiyo Sunzu alipewa kadi ya njano na mwamuzi Issa Kangabo kutoka Rwanda kwa kumchezea vibaya Tchechte. Mwanzoni mwa kipindi cha kwanza Uhuru Selemani alipoteza nafasi mbili za kufunga baada ya kuwatoka mabeki wa Azam, lakini jitihada zake ziliishia mikononi mwa kipa Deogratius Munishi, huku Azam wakijibu mapigo dakika 14 baada ya Kipre kuwatoka mabeki wa Simba na kupitisha pasi kwa Hamis Mcha aliyepiga fyongo shuti lake. Dakika ya 17 beki Shikanda wa Azam alipokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na kupiga krosi iliyotua kichwani kwa Bocco ambaye alipiga kichwa kilichokwenda wavuni na kumwacha Kaseja akiwa amesimama. Simba walijaribu kurudi mchezoni, lakini mashuti ya Kapombe na Mwinyi Kazimoto dakika 34 na 36 yalishindwa kulenga goli. Dakika 41 mwamuzi aliinyima Simba penalti baada ya Kazimoto kumuangusha Ramadhan Chombo kwenye eneo la hatari. Azam walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 46 kupitia Boko aliyemalizia vizuri kazi ya Tchetche aliyekuwa mwiba kwa ngome ya Simba. Mchezaji bora wa mwaka wa Taswa, Kapombe aliifungia Simba bao dakika 53 akipokea krosi ya Haruna Shamte na kupiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lililomshinda Munishi. Kocha wa Azam, Stewart Hall aliwapumzisha Tchetche, Mcha na kuwaingiza George Odhiambo na Jabir Aziz, wakati Simba ilimtoa Uhuru, Jonas Mkude, Mudde Musa na kuwaingiza Kigi Makasi, Amri Kiemba na Hamis Kinje. Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na faida kwa Azam kwani dakika 73, Aziz alitoa pasi kwa Boko na kupiga shuti la chini akiwa nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kuwanyamazisha kabisa mashabiki wa Simba. Awali Atletico ya Burundi inayosifiwa kwa kucheza soka ya kuvutia iliyaaga mashindano hayo kwa kuchapwa mabao 2-1 na AS Vita ya DR Congo. Mshambuliaji Etekiama Taddy alifunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo alipozifumania nyavu za Atletico katika dakika ya 8 na kuifanya AS Vita kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0. Atletico ilirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika 48 kwa shuti kali lililopigwa naPierre Kwizera akiitumia vizuri pasi iliyopigwa na Henry Mbazumutima. Wakati mashabiki wakidhani mpira huo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, mshambuliaji Basilua Makola aliifungia AS Vita bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-1. Nusu fainali ya michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa Azam kuivaa AS Vita saa nane mchana na mabingwa watetezi Yanga kupepetana na APR saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. |
kADA WA CCM AFUNGWA JELA KWAJILI YA KULA PESA ZA EPA
Send to a friend |
Mahakimu wawili katika jopo la waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo waliwatia hatiani watuhumiwa kwa makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa. Kwa upande wake kiongozi wa jopo hilo, Jaji Fatuma Masengi aliwaachia huru washtakiwa hao kwa maelezo kwamba upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka yote saba yaliyokuwa yanawakabili. Hata hivyo, hukumu hiyo haikuweza kuwaokoa watuhumiwa na hasa Farijala na Maranda watatumikia adhabu yao kwa miaka mitatu jela kwa kuwa adhabu zote walizopewa zitakwenda kwa wakati mmoja. Tayari Maranda na Farijala wanatumikia kifungo kingine cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh1.8 bilioni za EPA, ambapo walihukumiwa na mahakama hiyo Mei 23, 2011. Jopo lagawanyika Jopo la mahakimu watatu lililokuwa likisoma hukumu hiyo liligawanyika na kusoma hukumu mbili tofauti, ambapo hukumu moja iliyoandaliwa na kusomwa na kiongozi wa jopo hilo, Jaji Masengi aliyewaachia huru washtakiwa. Hata hivyo, katika hukumu ya pili, iliyoandaliwa na Hakimu Projestus Kahyoza na mwenzake Catherine Revocate iliwatia hatiani washtakiwa katika makosa sita kati ya saba yaliyokuwa yakiwakabili, na kuwahukumu kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa. Hata hivyo, wakati wakisoma hukumu hiyo, mahakimu hao walisema badala ya washtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 18, hukumu yao itaenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Kabla ya hukumu Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, hakimu Kahyoza na mwenzake walipitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwamo mtaalamu wa maandishi, Joseph Mgendi ambaye aliweza kuangalia saini katika nyaraka halisi na zinazodaiwa kughushiwa, ikiwamo hati ya usajili ambapo alibainisha kuwa zilikuwa zimeghushiwa. Pia walipitia utetezi uliotolewa wa mshtakiwa Maranda, ambaye aliyakana mashtaka yote saba yanayowakabili na kwamba, alikataa katakata kuwa hakuwahi kula njama na kughushi hati ya usajili wa Kampuni ya Money Planners & Consultant. Hakimu Kahyoza alisema, Maranda alidai kuwa yeye hakuwahi kwenda Brela kusajili kampuni hiyo na kwamba, aliyewahi kwenda kusajili kampuni ni binamu yake, Farijala. Hakimu Kahyoza alisema, Maranda katika utetezi wake alisema yeye hakuwahi kughushi hati yoyote hivyo, haikuwa rahisi kwake kutoa hati iliyoghushiwa pia, hakuwahi kuiba fedha BoT na wala hakuwahi kujipatia fedha yoyote kwa njia ya udanganyifu. Kahyoza alifafanua kwamba, Maranda alidai mfumo uliotumika kuwaingizia fedha kwenye akaunti yao iliyopo katika Benki ya CBA uliendeshwa kihalali ndiyo maana, BoT hawakuwahi kulalamika hivyo, aliiomba mahakama imuone hana hatia. Akisoma utetezi uliotelewa na Farijala, Hakimu Kahyoza alisema, Farijala naye alikataa madai ya kughushi, kuwasilisha nyaraka bandia benki, kuiba fedha yoyote na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na aliiomba mahakama imwachie huru kwa sababu hana hatia. Yasiyo na utata Hakimu Kahyoza alisema kuwa mahakama ilibaini kuwapo kwa masuala yasiyokuwa na utata ambayo ni pamoja na kwamba Maranda na Farijala ni ndugu, waliwahi kufanya biashara pamoja na waliingiziwa fedha kwenye akaunti namba 0101379004 ya United Bank of Africa ambazo ni kiasi cha Sh2.2 bilioni. “Baada ya kuweka msingi huo, mahakama ilijiuliza je, washtakiwa walikula njama ya kuiibia BoT, walighushi hati ya usajili wa kampuni namba 150731, walighushi hati ya mkataba kati ya Kampuni ya Money Planners & Consultant na Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani, waliwasilisha nyaraka za kughushi benki, waliibia BoT na kwamba je, walijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,” alihoji Kahyoza. Hakimu huyo alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, hakuna utata kuwa hakuna mahali panapoonyesha washtakiwa ndiyo walikuwa wamiliki wa kwanza wa kampuni hiyo Money Planners & Consultant na kwamba majina yanayodaiwa kuwa ni wamiliki wa kampuni hiyo ya Thobias Kitunga na Paulo ni majina ya uongo na ya kufikirika. Alisema licha ya majina hayo kuwa ya kufikirika, mabadiliko ya kampuni hiyo ya Money Planners & Consultant hayakuwahi kufanyika na hata Brela hakuna kumbukumbu, hivyo saini zilizopo katika nyaraka za kampuni hiyo ikiwamo hati ya usajili ni za kughushi. Alisema sababu ya kuthibitisha hilo ni kwamba, ofisi ni ileile iliyopo Magomeni Mapipa, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 hata baada ya mabadiliko. “Hati hizo za usajili hazikusainiwa na Msajili wa Biashara toka Brela, Noel Shani bali zilisainiwa na washtakiwa wenyewe. Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 333 na 335 (c) (e) vimetufanya tufikie hitimisho kuwa washtakiwa walighushi nyaraka hizo,” alisema Hakimu Kahyoza. Alisema Maranda na Farijala walighushi hati ya mkataba ya Septemba 8, 2005, wakitumia majina ya Thobiasi na Paul na kwamba hati hiyo haikusainiwa na Kampuni ya Money Planners & Consultant. “Maombi ya kupewa fedha hizo Sh 2.2 bilioni, yalipitiwa na watu kadhaa wakiwamo Mwanasheria wa BoT na kupeleka kibali cha mwisho kwa Gavana aidhinishe malipo, hakuna hata mmoja aliyebaini kuwa katika hati ya mkataba kati ya Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani na Kampuni ya Money Planners & Consultant, haikuwa na saini ya Kampuni ya Money Planners & Consultant,” alisema. Aliongeza: “Kwa sababu hiyo inaonyesha wazi, washtakiwa ndiyo walighushi nyaraka hizo hivyo hati ya usajili wa kampuni hiyo, hati ya mkataba ni za kughushi.” “Tuna haki ya kuamini kuwa washtakiwa kwa kujua, walifanya hivyo kwa nia mbaya ya kuwasilisha hati hizo za kughushi CBA na baadaye BoT”, alisema Kahyozi. Alisema hakuna ubishi kuwa hakuwapo hata shahidi mmoja aliyewahi kuthibitisha kuwa washtakiwa hao waliwahi kuiibia BoT Sh 660,210,000. “Katika hili hatupo tayari kukubaliana na upande wa mashtaka kwa sababu halijathibitika”. Aliongeza kwamba, hakuna utata kuwa BoT iliweka kwenye akaunti ya washtakiwa zaidi ya Sh2.2 bilioni na kwamba, kiwango hicho cha fedha kiliwekwa baada ya washtakiwa kuwasilisha hati za kughushi katika benki hiyo kuu ikiwamo hati ya usajili na hati ya mkataba. Hakimu alisema kulikuwapo na maofisa wa juu BoT waliotakiwa walithibitishe hilo, lakini, Mwanasheria wa BoT yeye alikuwa anathibitisha uhalali wa hati hiyo ya mkataba ambayo haikusainiwa upande mmoja na Kampuni ya Money Planners kuwa, “Ina nguvu kisheria hivyo, inaweza kutumiwa na BoT kuhamisha au kuchukua fedha zinazoongelewa katika maombi ya washtakiwa”. Alifafanua hakimu, “Mwanasheria alimaanisha kuna watu wengine walithibitisha, sisi kwa mtazamo wetu ni ajabu kwa maofisa hao hata mmoja hakuwahi kuona katika hati ya mkataba hakuna saini ya Kampuni ya Money Planners. Tunajiuliza walimezwa katika huu mtego au walipumbazwa? Kama walipumbazwa, upumbazo huo ulikuwa ni wa hali ya juu na kujikuta wote wanaingia kwenye mtego huu.” alisema Hakimu Kahyoza. Aliongeza kwamba washtakiwa hao walifanya matendo hayo yote kwa nia mbaya na kuwafanya watu wengine, wawe sehemu ya kughushi. Kuhusu shtaka la kula njama, kwa ujumla maelezo yote yanaonyesha Maranda na Farijala, walikubaliana makazi ya ofisi yawe Magomeni, Mtaa wa Iramba nyumba namba 7 ambako ni nyumbani kwao, waliwasiliana, walikutana, walijadiliana hivyo walitenda kosa la kula njama. “Sisi hatuna sababu za kusitasita kuwa kweli washtakiwa walikula njama dhidi ya BoT. Ni kweli walikula njama,” alisisitiza Kahyoza. Jaji Masengi Kwa upande wake, Jaji Masengi aliwaachia huru washtakiwa wote kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuyathibitisha mashtaka yote saba yanayowakabili. Jaji Masengi alisema BoT ndiyo wangekuwa walalamikaji wakuu, lakini haikuwahi kulalamika kutoa fedha hizo zinazodaiwa kuibwa na washtakiwa wala Kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani. Kuhusu kughushi, alisema ushahidi uliotolewa haukutosheleza kuthibitisha kosa hilo na kwamba licha ya utetezi kuwa na upungufu lakini hakukuwa na sababu za kuwatia hatiani. Kabla ya hukumu Kabla ya kusomwa kwa hukumu ya Hakimu Khayoza na Hakimu Catherine, Wakili wa Serikali, Alapha Msafiri aliiambia mahakama kuwa washtakiwa siyo wakosaji wa mara ya kwanza, wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela katika kesi namba 1161 ya mwaka 2008. Msafiri aliiomba mahakama itumie kifungu cha 348 na 358 cha Makosa ya Jinai (CPA), kutoa amri Maranda na Farijala walipe fidia au warejeshe kiasi walichojipatia kwa njia ya udanganyifu. Wakili Majura Magafu, anayewatetea Maranda na Farijala, alidai kuwa ni kweli washtakiwa walitiwa hatiani lakini, isiwe kigezo cha kuwapa adhabu kali kwa sababu kesi namba 1163 na 1161 zilifunguliwa siku moja, zinahusu makosa ya aina moja isipokuwa zilipangiwa jopo tofauti. “Hii ni tofauti na mtu aliyetenda kosa akaachiwa halafu akafanya tena kosa lingine, pia mazingira ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa yalikuwa na utata kwa namna moja au nyingine na kwamba washtakiwa walitenda makosa bila ya kujua kama wanatenda makosa,” aliwatetea wakili huyo na kuongeza: “Kwa hiyo ni dhahiri, matukio hayo hayakufanyika kwa makusudi kwa asilimia 100, kwa kuwa wao waliamini ni halali lakini baadaye ilibainika kuwa si halai”. “Waheshimiwa washtakiwa wote wana matatizo ya kiafya, Farijala ana matatizo ya presha ya macho na Maranda ana tatizo la Figo, naomba kama mahakama itaridhia chini ya kifungu cha 38, ina mamlaka ya kuangalia mazingira ya utendwaji wa matukio, hali za watuhumiwa na kuwaachia kwa masharti maalumu kutokana na afya zao,”alisema Magafu. Pia aliiomba mahakama itamke wazi wazi kuwa adhabu watakayopewa washtakiwa kama itakuwa ni ya kifungo, inastahili kuanza lini kwa sababu kumekuwapo na utata wa sheria, kuwa ni lazima wamalize kifungo cha awali ndiyo waanze kingine. Kwa upande wa Hakimu Catherine Revocate, alisema wamejadiliana kwa kuangalia mazingira ya kesi, afya za washtakiwa na kwamba ni wakosaji wa mara ya kwanza kwa sababu kesi hiyo inasimama peke yake, katika shtaka la kwanza hadi la saba kasoro shtaka la sita waliloachiwa huru; washtakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kila kosa. Pia alifafanua kuwa badala ya washtakiwa hao kutumikia kifungo cha miaka 18 katika mashtaka sita yanayowakabili, kifungo hicho kitakwenda sambamba hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela. |
RAIS WA GHANA HAIAGA DUNIA JANA
Send to a friend |
Tuesday, 24 |
Mills amekutwa na mauti siku chache tangu aliporejea kutoka Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za mashirika ya habari ya kimataifa zilizotolewa jana jioni zilisema Rais huyo wa tatu wa Ghana aliugua ghafla juzi Jumatatu na alifariki jana mchana baada ya kuzidiwa. Shirika la Uingereza Reuters lilimnukuu mmoja wa wasadizi wa Rais Mills akisema kuwa rais huyo alikuwa amethibitika kufariki jana mchana. Habari zaidi zilisema kwa mujibu wa Katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama alikuwa akitarajiwa kuapishwa jana usiku kuchukua nafasi ya Mills ili kuongoza taratibu za mazishi ya mtangulizi wake. Katika siku za karibuni afya ya kiongozi huyo imekuwa ikiripotiwa kuzorota na mwaka huu pekee ameshakwenda Marekani mara tatu kwa ajili ya tiba. Mara ya mwisho alionekana hadharani nchini Ghana Juni 3 mwaka huu wakati alipokwenda kutemebelea eneo la ajali ya ndege, ziara ambayo ilizua minong’ono kutokana na wanachi kudai kuwa hakuonekana kuwa mwenye siha njema. Profesa John Evans Fiifi Atta Mills alizaliwa Julai 21, 1944 na aliapishwa kuwa Rais wa Ghana Januari 7, 2009 baada ya kuwa ameshinda uchaguzi dhidi ya mgombea wa kilichokuwa chama tawala Nana Akufo-Addo katika uchaguzi wa 2008. |
Monday, July 23, 2012
GARI NDOGO AINA YA TAX LIKIWA LIMEPATA AJALI ASUBUHI NDANI YA SONGEA KARIBIA NA CHUO CHA MATABIBU
Huu upande wa nyuma huku gari likiwa limenyanyuka tairi juu baada ya kupta ajali hiyo
Upande wa ubavuni huku kukiwa na damu kidopgo ambayo alijifutia dereva kabla ya kukimbia
Maeneo ya mbela gari lilikuwa limeingia kwenye msingi amabo upo maalumu kwajili ya kupitisha maji machafu
Plate namba ya gari hilo imetolewa kabaisaa na dereva alikimbia nayo moja kwa moja
Saturday, July 21, 2012
WEMA AVAMIWA NA MAJAMBAZI
SIKU chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba hiyo ya kisasa.
WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo na kuiba vitu mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme ndani ya gari (control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na madirisha (power window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma (side miller).
Vitu vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni ‘makapeti’ ya ndani na vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani ya geti hilo.
WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na uvamizi huo ambao umemfanya kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa akizingatia kuwa tukio hilo limetokea wakati nyumba yake ina walinzi wawili.
“Ni kweli nimeibiwa hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila mazingira ya kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana walinzi wangu wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?” alisema Wema kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea: “Sikuwa na namna kwao, nilikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe utatuzi wa jambo hili sambamba na kuwabananisha walinzi wangu ambao walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini kama geti la kutokea nje lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe. Lakini hili geti ni gumu, mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua masaa matano ambapo kungekuwa kumekucha.”
INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati ya Juni mwaka huu, staa huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, alitangaza kupitia runinga kwamba anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina kila kitu ndani.
Kwa mujibu wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya nyumba hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja wa Wema, Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na samani zake shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.
HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya Jumanne kuzungumzia tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi zilithibitisha Wema kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni majambazi.
Subscribe to:
Posts (Atom)